-->

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UCHUMBA.


USIHARAKISHE.
Usiharakishe na kukurupuka kutafuta mchumba kabla ya wakati muafaka.Pengine unaweza kujiuliza ni wakati upi ni muafaka kutafuta au kuwa na mchumba?ni wakati unapokuwa umekomaa kiroho, kiakili na kimwili umejitambua kikamilifu ulikotoka, mahali ulipo na unapokwenda na umetathimini kwa makini mipango na ratiba yako ya sasa na ya baadaye ndipo waweza kuchukua hatua hii mhimu katika maisha.
Wengi wamepuuzia hili na kukurupuka kutafuta mchumba bila kujitathmini na kuishia kwenye uasherati na usaliti vilivyowaletea huzuni na majuto badala ya furaha na ndoa takatifu. Biblia inasema “Ni nani katika ninyi Kama akitaka kujenga mnara asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama kwamba anavyo vya kumalizia asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi watu wote waonao wakaanza kumdhihaki…….” (Luka 14:28-30).
👉: USITAFUTE MCHUMBA KWA MSUKUMO KUTOKA NJE.🙏👇
Usitafute mchumba Kwa kuangalizia, kushawishiwa, kuiga au kusukumwa na ndugu, marafiki au washiriki wenzako, suala la kutafuta mchumba linapaswa kutoka ndani yako baada ya kujithamini na kuona kuwa ni wakati mwafaka na kupata sababu za msingi za kupata mchumba hatimaye kufunga ndoa.
👉: USITAFUTIWE MCHUMBA.
Vijana wa kiume na wa kike wanatakiwa kuwa makini sana katika suala hili, yakupasa uwe na orodha yako ya sifa unazozitaka, cha msingi zisipingane na neno la MUNGU, hizo zitakuongoza katika kutafuta mke au mme utayempenda na kumfurahia, fanya maamuzi ambayo hutakuwa na sababu ya kumfurahia mwingine.
Ushauri wa ndugu, jamaa, marafiki na viongozi wa kanisa unafaa kuzingatiwa kwa makini,lakini maamuzi ya mwisho yatoke kwa mhusika ambaye ataambatana na huyo mwenzi maisha yote, wengi wametafutiwa na kuishia kulaumu na kuvunja uchumba na hata ndoa.
✍️✍️ #MkakaFulani
💪
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU