Wakati mwingine una huzuni kwakua unakumbatia vitu ambavyo vinakuumiza kila wakati, unapokua na mtu ambaye hakuthamini na umefanya kila kitu ili akuthamini lakini haoni thamani yako ni wakati wa kujichagua wewe na kujipenda wewe. Iwe ni mke wako au mume wako kama hakuthamini na hajali chochote unachomfanyia ni wakati wako sasa wa kujijali.
Wakati mwingine watu hawaoni thamani yako kwakua hata wewe mwenyewe huoni thamani yako, unajidharau na kujidhalilisha, unajiona kama una kasoro nyingi na humshukuru Mungu kwa namna ulivyo. Unaweza kuwa una mapungufu lakini hivyo ndiyo ulivyo, kama mtu anakupenda basi atakukubali kutokana na mapungufu yako.
Lakini kama atatumia mapungufu yako kukuumiza basi jua huyo mtu hakupendi, sasa kama unaishi na mtu ambaye hakupendi kwanini wewe usijipende. Kwanini wewe usijithamini, huwezi kumlazimisha mtu kukupenda, kukuhaehimu wala kukujali lakini unaweza kujilazimisha, ukajipenda, ukajiheshimu na ukajijali, anza sasa kujijali na kujiona wa muhimu na kila mtu atakuona wa muhimu.