-->

BINTI YANGU NAOMBA USOME HII.


πŸ’˜"Mama anaongea na mwanawe na kumpa Usia"​
πŸ’˜Mwanangu mpenzi:
πŸ’˜Kuna siku utanikuta uzee, sitafanya mambo yangu kwa akili;
πŸ’˜Yakitokea hayo nakuomba tafadhali nipe muda na subira ili unifahamu !!​
πŸ’˜Pale mikono yangu itakapo tetemeka, na chakula changu kikaangukia kifuani pangu, na nisipoweza kuvaa nguo zangu;
πŸ’˜Jifunge na kusubiria, na kumbuka miaka imepita nilikuwa nakufunza ambayo leo siwezi kuyafanya!!​
πŸ’˜Ikiwa leo si maridadi na sina harufu nzuri; usinilaumu.. kumbuka udogoni kwako nikijitahidi sana nikufanye uwe maridadi mwenye harufu nzuri!!
πŸ’˜Usinicheke utakapoona ujinga wangu na kutofahamu mambo ya wakati wenu huu, lakini wewe kuwa jicho na akili yangu ili niyapate niliyoyakosa!!
πŸ’˜Mimi ndiye niliyekufunza adabu na mimi ndiye niliyekufunza vipi ukabiliane na maisha;
πŸ’˜Sasa leo unanifundisha yaliyo wajibu na yasiyo wajibu? ni kwa vile nimezeeka.
πŸ’˜Usinichoke kwa udhaifu wa kumbukumbu yangu, na uchelewaji wa maneno yangu na fikra zangu wakati ninapozungumza nawe, kwani furaha yangu wakati huu ni kuwa pamoja nawe tu!!
πŸ’˜Wewe nisaidie tu kupata ninachohitaji; kwani bado najua ninachotaka!!
πŸ’˜Miguu yangu ikikataa kunipeleka sehemu ninayotaka kwenda; nihurumie na kumbuka kwamba mimi nilikushika sana mkono ili uweze kutembea!!
πŸ’˜Usione haya abadan kunishika mkono wangu leo; kwani kesho utatafuta wa kukushika mkono wako!!
πŸ’˜Katika umri wangu huu; elewa kuwa mimi siyaelekei maisha kama wewe; lakini kwa ufupi nangojea mauti; kwa hiyo kuwa pamoja nami wala usinitupe!!​
πŸ’˜Pale ukikumbuka makosa yangu; jua kuwa mimi nilikuwa sitaki ila maslahi yako!!
πŸ’˜Na mimi napenda sana unayonifanyia hivi sasa kwa kunisamehe matelezo yangu na kusitiri aibu zangu..​
πŸ’˜Bado vicheko na tabasamu zako vinanipa furaha kama ulivyokuwa mdogo... kwa hiyo usininyime suhuba yako!!
πŸ’˜Nilikuwa nawe wakati unazaliwa; jitahidi kuwa karibu nami pale nitakapofariki!!​
πŸ’˜πŸ’˜NAWE MOLA AKUGHUFIRIE NA AKUSTIRI!!πŸ’˜πŸ’˜
πŸ’˜Maneno bora yaliyopitia katika maisha yangu, na hata nikiyarudia mara elfu moja, sichoki kuyasoma.."Mola wangu warehemu wazazi wangu kama walivyonilea nilipokuwa mdogo.
​πŸ’˜MANENO MAZITO KWA MWENYE AKILIπŸ’˜
Share:

Popular Posts

Blog Archive

Copyright © UTAMU KITANDANIDESIGNED BY TEETOU