idd makengo
Kamani mwanamke na una hela zako, kumzidi mpenzi wako au mko sawa lakini unapenda tu kutoa, hembu nikuambie kitu, kabla ya kuumia na kuja kulia huko baadaye hembu acha kumhonga mpenzi wako kwakua unadhani kuwa atakuoa. Mmekaa kwenye mahusiano muda mrefu labda hata kwenu anafahamika na mahari labda ashaleta wewe ushajiozesha.
Unasema huyu wangu hivyo chako chake chake chako. Dada yangu kama hajakuoa hata kama mshazaa na watoto huyo si mume wako. Narudia kama hajakuoa si wako hivyo anaweza kukucha, sasa utajiuliza vipi naweza kumhudumia, kumpa pesa na kumhonga. Jibu ni ndiyo si unazo, lakini usifanye hivyo eti ukidhani atakuoa.
Hapana fanya hivyo kama wanaume, wanaume wengi achana na wale ambao wanapenda sijui kama nini, wale wengi sana, anapomhonga mwanamke hela si kwasababu atamuoa, hata si kwasababu anampenda, wengi nikwakua anazo, anataka kuonyesha uanaume wake na anadhani ni jukumu lake au hataki tu kelele za kulialia kila siku na wala hana mpango wa kumuoa.
Ndiyo maana mwanaume anaweza kuwa na wanawake kumi lakini kama tabia yake ni ya kuhonga akawahudumia wote halafu asioe hata mmoja. Hivyo kama una jamaa yako, unataka kumdekeza awe kama mke wako, Dada yangu mhonge tu kwakua unazo na huna ndugu wa kuwasidia au huwezi kununua kiwanja ukajenga lakini si kumhonga kwakua eti atakuoa!
Hapana kwanza mwanaume wa namna hiyo ni ngumu kukuoa kwakua anajua hawezi ku kucontrol, kwa mwanaume control ni kila kitu akishajua hawezi kukucontrol ngumu kukuoa atataka aoe wa chini yake, lakini pili si lazima akuoe. Wema wako haumaanishi ubadilishane na ndoa, kumpa pesa si kama unanunua ndoa, wewe mpe tu kwakua kitandani anakufanya kuimba kikwenu lakini si kwakua unasema tu eti atanipoa.
Akikuoa baadaye shukuru Mungu ila kama ndiyo lengo lako, eti umpe hela mpaka akuoe Dada yangu badili malengo na mbinu kwani kwa wanaume waliokamilika achana na hawa wanaume Kaptula pesa si kigezo kabisa cha kumuoa mwanamke. Sasa nimalizie kwa kusema Dada yangu wewe endelea na roho yako nzuri lakini acha kuwaza ukidhani eti ukitoa hela nyingi ndiyo utaolewa! Hapana utaishia kuumia tu!
Toa hela kama anashida, kama unazo, kama unataka na kama akikuoa mshukuru Mungu lakini sio unatoa halafu unataka kulazimishia ndoa. Au unatoa anakuacha unaanza kulia ohhh Mungu atanilipia kanilia pesa zangu, nilimchukulia mkopo! Dada yangu ni wapi Mungu alisema ununue ndoa mpaka leo useme atakulipia, sisemi msihonge, hongeni tu Dada zangu hali ngumu hata wanaume tunalia na hii hali ila honga hela ambayo unaweza kusamehe!
Kwamba hata akikucha hutalia sana, lakini umemchukulia mkopo, kajenga nyumba au gari na kesho kakuacha halafu unapita unakuta analiendesha au kaoa na mwanamke mwingine anaishi katika nyumba uliyomjengea, daa Mungu anakuona! Nikukumbushe tu wote walioachwa walikua wanapendwa kama wewe ndiyo maana waliwaamini mpaka kuwapa kila kitu, hivo wewe jidanganye kuwa hawezi niacha naanipenda sana wakati wewe ni N0. 3 wake.
NISIWAKATISHE TAMAA; Hongeni Tu! Nikama Sadaka Au Fungu La Kumi!